Mkono Vision



Shule ya MVS ni shule ya kutwa na bweni yenye usajili No: XXXX inakutangazia nafasi za masomo za Pre-form ONE kwa ajili ya maandalizi wa muhula mpya wa masomo unaoanza January mwaka 2020. Shule ni MPYA na inaanza kidato cha kwanza mwaka 2020.

Secondary School

Maabara ya Kisasa

Eneo Tunapopatikana





Shule ya sekondari ya Mkono Vision ipo mjini KATORO umbali wa KM 2.5 upande wa Magharibi ya Mji. Mji wa KATORO upo katika Wilaya ya Geita umabali wa KM 42 kutoka Mjini Geita. Huduma ya usafiri wa Tax inapatikana kwa Tsh 5,000/=, na bajaji Tsh 2,000/= na bodaboda Tsh 1,000/= kutoka kituo cha mabasi Katoro.

Mazingira Ya Shule

SShule ina mazingira mazuri ya kumwezesha mwanafunzi kusoma na kufaulu vizuri masomo yake. Shule ina Maktaba na Maabara ya kisasa kwa masomo yote ya sayansi na Kompyuta iliyoandaliwa maalum kuwasaidia watoto kuenenda na dunia ya UTANDAWAZI. Pia, shule ina waalimu wazuri wenye uzoefu waliobobea katika ufundishaji na malezi bora kwa Watoto wa JINSIA zote.

Jinsi ya Kujiunga

Shule ni ya KUTWA na BWENI na inachukua Wanafunzi wa KiKE na wa KIUME. Gharama za kujiunga na shule kwa mwaka ni Shs 2,000,000/= kwa Wanafunzi wa Bweni (boarders). Hii ikiwa imejumuisha ada ya shule (Shs. 1,800,000) na michango mengineyo (Shs.200,000). Kwa Wanafunzi wa kutwa (day scholars) ada ni Shs 1,050,000/=. Hii ikiwa imejumuisha ada ya shule (Shs. 900,000) na michango mengineyo (Shs.150,000) Malipo yote yalipwe kupitia akaunti ya Shule No. XXX iliyopo katika Benki ya XXX. Maelezo mengine juu ya mahitaji muhimu ya Mwanafunzi wa KUTWA na wa BWENI yanapatikana katika TOVUTI ya Shule XXXX .


Malengo Ya Shule Yetu

Nia ya kuanzisha shule yetu ni kuwapatia malezi na elimu ya sekondari hasa wasichana wanaoshindwa kuvipata sehemu nyingine kutokana na hali ngumu ya uchumi.

Maono Yetu

Maono ni picha ya tukio au kitu Fulani kinachoonekana kwa dhahiri wakati mtu akiwa na ufahamu .Mahubiri ya Jumapili: Maono ya kiungu au nguvu ya maono .... Haya yakifanyika shule za kata zitatamba kitaaluma.

Shule yetu ni chaguo bora kwa mwanao

Jiunge Sasa Nafasi ni Chache

Fomu za kujiunga zinapatikana Shuleni
Kwa mawasiliano zaidi, tumia namba zifuatazo;
Tel: 0786398 882
0764796682

At MVSS, Education never ends, it only begins